Gossip

Willy Paul Amkosoa Jalang’o kwa Kumtema Luo Festival

Willy Paul Amkosoa Jalang’o kwa Kumtema Luo Festival

Mwanamuziki Willy Paul ameonyesha kukerwa na hatua ya mbunge wa Lang’ata, Phelix Odiwuor maarufu Jalang’o, ya kutomualika kutumbuiza kwenye tamasha la Luo Festival iliyofanyika wikiendi hii iliyopita.

Kupitia ujumbe wake mtandaoni, Willy Paul ameonekana kushangaa na kuhoji sababu ya kuachwa nje ya orodha ya wasanii waliopangwa kutumbuiza, akisisitiza kuwa ana uhusiano wa karibu na jamii ya Wajaluo na alipaswa kupewa nafasi kwenye hafla hiyo.

Tukio hilo limezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimtaka Jalang’o kuzingatia vipaji mbalimbali bila kujali kabila au historia ya msanii, huku wengine wakieleza kuwa huenda kulikuwa na sababu za kiutendaji zilizosababisha msanii huyo kutoalikwa.

Luo Festival ni moja ya matukio makubwa ya burudani yanayoandaliwa kila mwaka, yakileta pamoja maelfu ya mashabiki wa muziki na burudani kutoka pembe mbalimbali za nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *