
Staa wa muziki nchini Willy Paul amejizawadi gari aina ya Mercedes-Benz C-Class ambapo inatajwa kuwa ametoa kiasi cha takriban shilling millioni 6 kuinunua.
Kupitia ukurasa wake instagram mkali huyo wa tamu wallahi ameshare video fupi ikionyesha muonekano wa gari hilo huku akisema amechukua hatua ya kujizawadi kutokana na mafanikio makubwa ambayo anazidi kupata kwenye kazi zake za sana.
Lakini pia amewashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono na kumuonyesha upendo kwenye muziki wake huku akiahidi kuachia nyimbo kali zenye maudhui safi mfululizo bila kupoa.
“God did it again!!! Glory be to the most high God.. thank you my father for yet another beautiful gift… Decided to gift myself for the good job I’ve been doing.. for the CLEAN CONTENT I’ve been releasing… I intend to keep it that way… and to you my fans that gave me a second chance Asanteni. It is because of your generosity that I am where I am today…
Another mercedesbenz double sunroof hehe” Ameandika Instagram.
Kauli yake inakuja baada ya kutokea kwenye orodha ya wasanii kumi waliotizwa Zaidi katika mtandao wa youtube nchini ambapo kwenye orodha hiyo iliyotawalia na wanamuziki kutoka Nigeria na Tanzania alikamata nafasi ya saba na kuwa msanii pekee kutoka Kenya aliyepata mafanikio hayo.