Entertainment

Willy Paul atamani kuingia kwenye ndoa

Willy Paul atamani kuingia kwenye ndoa

Msanii Wily Paul ameshindwa kujizua mtandaoni baada ya kukiri hadharani kuwa anatamani kuingia kwenye ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshea video hii ikionesha vitu vya thamani ambavyo vipo ndani ya nyumba yake ya kifahari na kusindikiza na ujumbe wenye mafumbo unaoashiria kuwa amechoshwa na maisha ya upweke.

“Just one step left for you to enjoy all these with me, just say YES I DO … let’s grow old together”, Aliandika.

Posti yake hiyo imeonekana kuzua gumzo miongoni mwa wafuasi wake, wengi wakionekana kumtakia mema kwenye harakati za kumtafuta mwanamke wa ndoto yake huku wengine wakiichukulia kama mzaha kutokana na matukio ya kuigiza ambayo amekuwa akitengeneza kwenye mitandao ya kijamii.

Utakumbuka Bosi huyo wa “Saldido” hajawahi kuweka wazi mahusiano yake kwa umma, licha ya kujitapa mtandaoni kuwa ana mke na watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *