Entertainment

Willy Paul Awataka Mashabiki Wamsaidie Kuchagua Location ya Video Mpya

Willy Paul Awataka Mashabiki Wamsaidie Kuchagua Location ya Video Mpya

Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Willy Paul, ametangaza kuwa kwa sasa yuko katika harakati za kutafuta eneo bora la kupigia video ya wimbo wake mpya.

Kupitia mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo alisema kuwa ana mipango mikubwa ya kuhakikisha video hiyo inakuwa ya kiwango cha juu, na hivyo anahitaji mandhari ya kuvutia itakayoendana na ubora wa kazi yake.

“Natafuta location kali ya kushoot music video. Mnaweza nisaidia na ideas?” aliandika Willy Paul.

Mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi na kutoa mapendekezo tofauti, baadhi wakimtajia maeneo kama: Ngong Hills, The Alchemist, Westlands, Karura Forest, Watamu au Diani Beach na Nairobi Railway Museum.

Willy Paul, ambaye hivi majuzi amekuwa akizua gumzo kutokana na mabadiliko ya kimuziki na mitindo, anaonekana kutaka kupeleka ubunifu wake kwenye kiwango kingine. Wimbo huu mpya unatarajiwa kuwa sehemu ya mradi mkubwa anaotarajia kuuzindua kabla ya mwisho wa mwaka.

Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni eneo gani atakalochagua na iwapo video hiyo itavunja rekodi kama kazi zake za awali