
Staa wa muziki nchini Kenya Willly Paul amefichua kiasi cha fedha anayohitaji ili aweze kushiriki kwenye reality show.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema analipisha kiasi cha shilling milioni 100 za Kenya kwa kampuni au mtu yeyote anayehitaji huduma zake kwenye reality show yeyote ile.
Hitmaker huyo wa “Tamu Wallahi” amesema yeye sio mtu wa kupenda reality shows kwa kuwa ana kipaji cha kipekee kwenye muziki, hivyo atatoza kiasi hicho cha pesa kutokana na brand yake muziki ambayo inazidi kukua kila uchao.
Willy Paul amewashauri wasioweza kufanya naye kazi kutafuta chapa zingine ambazo watamudu gharama zao kwani hana mpango wa kupunguza bei yake mwaka huu.
Hata hivyo amewatoa uvivu baadhi ya wasanii wanaongoja atoe wimbo ndio waweze kuachia kazi zao kwa kusema kuwa mwaka 2023 hataki kushindana na msanii yeyote bali ataachia kazi zake kulingana na ratiba yake.