 
									Staa wa muziki nchini Kenya, Willy Paul, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mahusiano ya kimapenzi, akisema hawezi kamwe kuwa na uhusiano na mwanamke mlevi.
Kupitia ujumbe aliouweka mtandaoni, , Willy Paul amesema kuwa anapendelea kubaki single kuliko kujihusisha kimapenzi na mwanamke anayependa pombe kupita kiasi.
Mkali huyo wa ngoma ya Ngunga, amesema wanawake wa aina hiyo mara nyingi hawana nidhamu wala mwelekeo wa maisha, jambo analoliona halifai kwa mtu anayemtafuta mwenza wa kweli.
Hata hivyo ameongeza kuwa anaomba Mungu amuepushe na wanawake wenye tabia za ulevi, akisisitiza kuwa heri abaki bila mpenzi kuliko kuwa na mwanamke mlevi.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            