
Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize anaendelea kuchukua headlines mbalimbali mara baada ya wimbo wake wa Mwaka Wangu kutajwa na kuchezwa katika ibada kwenye moja ya kanisa mkoani Arusha inayoongozwa na Mchungaji Geor Davie.
Mtumishi huyo ambaye anajulikana kama Nabii Geor Davie , ameuelezea wimbo huo kama wimbo mzuri usio na maneno mabaya , na kumtamkia Harmonize maneno ya baraka na kumshahuri kuokoka kabla ya kurusu wimbo huo kupigwa na kuchezwa katikati ya ibada siku ya juma pili Februari 21.
Hata hivyo Harmonize ameonekana kukoshwa na hatua ya wimbo wake wa mwaka wangu kuchezwa kanisani ambapo ameahidi kutembelea kanisa hilo hivi karibuni.
Ikumbukwe kuwa Harmonize pia ametoa wimbo wa injili uitwao ‘Omoyo Remix’ alioimba na mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za injili Jane Misso ndani ya mwezi huu..