Gossip

WINNIE NWAGI AWACHANA WAKOSOAJI WA MAVAZI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

WINNIE NWAGI AWACHANA WAKOSOAJI WA MAVAZI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi amemtolea uvivu wanaokosoa uvaaji wake wa mavazi kwenye mitandao ya kijamii.

Akipiga stori na runinga moja nchini Uganda Winnie Nwagi amewataka wanaochukia mtindo wake wa mavazi wampe kazi ya kumuingizia kipato ili avae mavazi wanazozipenda.

Hitmaker huyo wa “Kwata Essimu” amesema hayupo dunia kumfurahisha mtu yeyote ila yupo kwa ajili ya kumfanya binti yake awe mwenye furaha zaidi ambapo amewataka wanaomtusi kwenye mitandao ya kijamii wajipe shughuli zitakazowaingizia hela badala ya kufuatilia maisha yake.

Itakumbukwa Winnie Nwagi amekuwa gumzo nchini Uganda kutokana na mtindo wake wa mavazi yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *