Entertainment

WIZKID AMZAWADI GARI MENEJA WAKE SUNDAY ARE

WIZKID AMZAWADI GARI MENEJA WAKE SUNDAY ARE

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid ameufunga mwaka 2021 kwa kujiongezea baraka, amemfanyia surprise meneja wake wa muda mrefu Sunday Are kwa kumpatia zawadi ya gari mpya aina ya Prado.

Meneja huyo ameshare video kwenye Instagram kuionesha gari hiyo, Toyota Land Cruiser SUV na kumshukuru Hitmaker huyo wa Essence.

Thamani ya gari hiyo ni kati ya shilingi milioni 6.9 hadi milioni 10 za Kenya kulingana na mahali na jinsi ilivyonunuliwa.

Hii si mara ya kwanza Sunday anapewa zawadi ya gharama na staa huyo. Mwaka 2019 Wizkid alimpa zawadi saa ya Richard Mille.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *