Entertainment

Wizkid aomba radhi mashabiki kwa kususia show

Wizkid aomba radhi mashabiki kwa kususia show

Staa wa muziki nchini Nigeria Wizkid ameomba msamaha mashabiki zake wa Ghana kwa kushindwa kutokea kwenye show yake mjini Accra nchini Ghana siku ya Jumamosi licha kutua nchini humo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii amesema kwamba kuna mambo hayakuwa sawa hasa upande wa kiufundi na usalama wake. Pia ameongeza kwamba, muda wowote atatangaza tarehe mpya ya kufanya show hiyo.

Katika hatua nyingine mkali huyo pia hakutokea kwenye show yake aliyokuwa aifanye jana Jumapili huko Abidjan nchini Ivory Coast, na inatajwa kuwa alikuwa tayari ametua nchini humo ila kwenye show hakutokea.

Tukio hili bado halijatolewa ufafanuzi na uongozi wa mkali huyo, ila taarifa iliyopo hadi sasa, uongozi wake unashikiliwa na Polisi mjini Abidjan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *