Entertainment

WIZKID AWAPONGEZA BLACK COFFEE NA ANGELIQUE KIDJO KUSHINDA GRAMMY

WIZKID AWAPONGEZA BLACK COFFEE NA ANGELIQUE KIDJO KUSHINDA GRAMMY

Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid amewapongeza Waafrika wenzake Angelique Kidjo kutoka Benin na Black Coffee kutoka Afrika Kusini ambao waliibuka washindi kwenye tuzo za 64 za Grammy, ambao alikua akichuana nao kwenye vipengele tofauti tofauti.

Wizkid ametoa pongezi hizo kwa wasanii hao kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram huku Wanigeria wakiwa bado na dukuduku kuwa msanii wao (Wizkid) ndio alistahili zaidi kupewa tuzo hizo.

“Hongereni sana kwa kuendelea kuling’arisha bara la Afrika. Muziki wa Afrika unakua”, Ameandika WizKid.

Ikumbukwe, Wizkid alitajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za grammy kupitia vipengele vya Best Global Music Perfomance na ngoma yake ya Essence) na Best Global Music Album na album yake Made In Lagos: Deluxe Edition).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *