
Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria Wizkid ameendelea kuweka rekodi haswa upande wa namba kwenye digital platforms mbalimbali.
Taarifa njema kwa mashabiki wa staa huyo ni kwamba ameweza kuwa mwanamuziki wa kwanza Africa kupata zaidi ya streams billion 1 katika mtandao wa Apple Music.
Wizkid pia amefikisha watazamaji millioni 1.3 YouTube , streams millioni 1.16 katika mtandao wa Spotify , jumla ya streams million 349 (total streams) Audiomack, streams 183 million Pandora na streams million 126 Boomplay.