
Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid anaendelea kutupasha kuhusu album yake mpya ijayo aliyoipa jina la “SeiLess”.
Kupitia insta story yake ameeleza itaachiwa kati ya mwaka huu 2022 au mwanzoni mwa 2023.
Ikumbukwe, “SeiLess” inaenda kuwa album ya SITA ya Wizkid baada ya “More Love, Less Ego” ambayo imetoka wiki mbili zilizopita ikiwa ni album ya TANO.
Album zingine za WizKid ni Superstar (2011), Ayo (2014), Sounds from the Other Side (2017) na Made in Lagos (2020).