Entertainment

YKEE BENDA APINGA UCHAGUZI WA UMA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

YKEE BENDA APINGA UCHAGUZI WA UMA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Mwanamuziki kutoka Uganda Ykee Benda amepinga hatua ya Chama cha Wanamuziki nchini humo UMA kutaka kufanya uchaguzi kwa njia ya mtandao.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Ykee Benda amesema upigaji kura ukifanyika mtandaoni hatokuwa na uwazi kwa sababu matokeo yanaweza kubadilishwa na watu wanaosimamia maswala ya mitandao.

Msanii huyo ambaye alikuwa rais wa zamani chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA amependekeza uchaguzi wa chama hicho kuandaliwa kwa mfumo wa kawaida wa watu kupiga foleni kwenye vituo vya upigaji kura.

Hata hivyo ameutaka uongozi wa UMA kuomba usaidizi wa kifedha kutoka kwa mashirika ya kijamii na serikali kufadhili maandalizi ya uchaguzi wa kuwateua viongozi wapya wa chama hicho kama kweli hawana pesa za kutosha za kuandaa uchaguzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *