
Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records msanii Ykee Benda ameitaka serikali ya Uganda kuiweka Februari mosi ya kila mwaka kuwa Sikikuu ya Kitaifa kumkumbuka Marehemu Mozey Radio ambaye alifariki tarehe hiyo mwaka wa 2018.
Akizungumza huko Kagga nchini Uganda ambako Mozey Radio alipumzishwa mwaka wa 2018, Ykee Benda amesema mwendazake mozey Radio alikuwa nguzo muhimu katika taifa la uganda, hivyo ni vigumu kujaza pengo aliloliacha kwenye tasnia ya muziki nchini humo.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Obangaina” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi anachipukia kwenye tasnia ya muziki nchini uganda alikuwa na mazoea ya kuiba mashairi ya nyimbo za mozey Radio na kuyatumia kwenye nyimbo zake.