Entertainment

YKEE BENDA AWAPA CHANGAMOTO MAPROMOTA WA MUZIKI KUWAPA WASANII WA NDANI KIPAU MBELE KWENYE SHOWS ZAO.

YKEE BENDA AWAPA CHANGAMOTO MAPROMOTA WA MUZIKI KUWAPA WASANII WA NDANI KIPAU MBELE KWENYE SHOWS ZAO.

Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records, Ykee Benda ametoa wito kwa mapromota wa muziki nchini uganda kutowapa wasanii wa nigeria kipau mbele kwenye shows zao.

Ykee Benda amesema tangu Rais Yoweri Museveni afungua uchumi wa nchi ya Uganda mapromota wengi nchini humo wamekuwa na mazoea ya kuwapa nafasi wasanii wa Nigeria kwenye shows zao huku wasanii wa ndani wakisahaulika.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Obangaina” amesema mapromota wa muziki  hawawatendei haki wasanii wa Uganda kwa kuwanyima shows ikizingatiwa kuwa hawajatumbuiza kwa kipindi cha miaka miwili tangu ujio wa Corona.

Hata hivyo mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda wamewataka wawekeze kwenye kazi zao za muziki kwani wengi wamekuwa wakiachia nyimbo ambazo hazikithi vigezo vya kimataifa wakiwa na imani kuwa zitafanya vizuri sokoni.

Katika kipindi cha wiki mbili iliyopita,wasanii wawili wa nigeria chike pamoja na Ruger wamefanya shows kali nchini uganda huku wasanii wengi kutoka nigeria wakitarajia kuzuru uganda kwa ajili ya shows zao hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *