
Rapa kutoka Marekani Young Thug yupo korokoroni tangu mwezi Mei mwaka huu, hii imepelekea kuharibu baadhi ya mipango yake mingi ikiwemo kutofanyika kwa maonesho ambayo tayari alikuwa ametakiwa kuyafanya.
Kwa mujibu wa The Atlanta Journal Constitution, Thug amefunguliwa mashtaka na promota wa kampuni ya A-1 Concert Entertainment kwa kutofanya onesho ambalo alitakiwa kufanya mwezi June mwaka huu. Waandaaji hao wanataka alipe pesa yao ya utangulizi kiasi cha shilling million 17.9 za Kenya.
Ripoti zinasema, Thug alitafutwa mwezi January kwa ajili ya makubaliano ya kufanya show hiyo ya dakika 45 kwa malipo ya shilling million 35.9 lakini kuwa kwake Jela hadi leo kumemfanya kutotimiza makubaliano ya kutumbuiza.