Tech news

YouTube Yazindua Kipengele Kipya cha “Recap” Kama Spotify Wrapped

YouTube Yazindua Kipengele Kipya cha “Recap” Kama Spotify Wrapped

YouTube imeanza kufanana na majukwaa kama Spotify, YouTube Music na Apple Music baada ya kuzindua kipengele kipya cha YouTube Recap, ambacho kitaonyesha muhtasari wa shughuli zako zote kwenye YouTube kwa mwaka mzima.

Kupitia YouTube Recap, watumiaji wataweza kuona: Channels walizotazama sana, YouTube Shorts zilizopendwa zaidi, Aina za content wanazovutiwa nazo, Historia fupi ya matumizi yao ya YouTube kwa mwaka husika.

Kipengele hiki kimeanza kujionyesha kwa baadhi ya watumiaji tangu jana, na YouTube imethibitisha kuwa ndani ya wiki hii, kitapatikana kwa watumiaji wote duniani.

Mara tu kitakapopatikana kwenye akaunti yako, utapata YouTube Recap ndani ya sehemu ya “You” tab, ambapo utapata ripoti yako ya mwisho wa mwaka kama ilivyo kwenye huduma nyingine za muziki.

Kipengele hiki kinatarajiwa kuongeza ushiriki wa watumiaji na kuwapa nafasi ya kuelewa zaidi tabia zao za kutazama video kwenye jukwaa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *