Gossip

YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

Mchekeshaji maarufu wa Kenya, YY Comedian, amefichua kisa cha kushangaza kuhusu maisha yake ya mapenzi ya zamani.

Akizungumza katika kipindi cha Feast with Friends kinachoendeshwa na Shiksha Arora, YY alieleza kuwa aliwahi kumtema mwanamke mara baada ya mkutano wao wa kwanza kwa sababu alishindwa kutandika kitanda.

Kwa mujibu wa msanii huyo, tukio hilo lilimfanya atathmini mitazamo na maadili ya mpenzi wake, jambo lililomsukuma kufikia uamuzi wa haraka wa kumaliza uhusiano. YY alisema kwake nidhamu na mpangilio ni mambo ya msingi katika maisha ya kila siku, na kushindwa kwa mwanamke huyo kutandika kitanda kulionekana kama ishara ya kutopenda usafi na kutojali mambo madogo.

Kisa hicho kimezua mijadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakiona sababu hiyo kuwa ndogo mno kupelekea kuvunja uhusiano, huku wengine wakimtetea wakisema kila mtu ana haki ya kuweka viwango vyake vya maisha binafsi.

YY Comedian amejulikana kwa ucheshi wake wa kipekee na mara nyingi hutumia matukio ya maisha binafsi kama chanzo cha vichekesho, jambo linalomfanya kuendelea kuwa miongoni mwa wakali wa tasnia ya ucheshi nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *