Gossip

Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Socialite maarufu wa Uganda, Zari Hassan, ameripotiwa kumshauri mumewe Shakib Cham kuachana na mchezo wa masumbwi na kuelekeza nguvu zake katika shughuli nyingine za kibinafsi zinazoweza kumuingizia kipato.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wawili hao, Zari amekuwa mstari wa mbele kushauri mumewe kutokana na hali iliyoonekana baada ya pambano la hivi karibuni lililomshirikisha Shakib na msanii Rickman Manrick.

Katika pambano hilo, Shakib alipokea makonde mazito ya kichwa yaliyopelekea kuanguka chini na kupoteza fahamu, hali iliyomlazimu muamuzi kusitisha pambano hilo mara moja.

Tukio hilo lilimuumiza mno Zari ambaye alishuhudia mumewe akizirai ulingoni na kulia machozi ya uchungu. Chanzo hicho kimeeleza kuwa, licha ya juhudi za Shakib kujaribu kujiweka kwenye tasnia ya masumbwi ya burudani, mchezo huo haujaweza kuleta mapato yaliyotarajiwa na badala yake umekuwa chanzo cha hofu na maumivu kwa familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *