
Msanii wa Dancehall kutoka nchini Uganda Ziza Bafana amejiunga na orodha ndefu ya wasanii ambao hawataki Cindy Sanyu arejee afisini kama Rais wa Muungano wa Wanamuziki nchini humo (UMA) kwa muhula wa pili.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Uganda, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Speed Controlle” amesema anamuunga mkono King Saha kuwa rais wa muungano huo kwa kuwa Cindy amefikia kiwango anachohitaji kuzingatia zaidi majukumu yake ya kifamilia.
“Tumemuinua. Amefanya makubwa. Sasa mwache arudi nyumbani akalee watoto wake. Nampenda kama dada, lakini namuunga mkono King Saha,” amesema
Ziza Bafana ameenda mbali zaidi na kusema kwamba UMA inahitaji kiongozi shujaa na jasiri kufanikisha malengo ya muungano huo tofauti na Cindy ambaye amekuwa akikatishwa tamaa na maneno ya watu mtandaoni.
Utakumbuka Cindy Sanyu atachuana na King Saha pamoja na Maurice Kirya kwenye kinyanganyiro cha kugombea urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.