
Msanii wa Dancehall Ziza Bafana amewahimiza wanawake kutia bidii na kuwasaidia waume zao katika malezi ya familia.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Bafana ameeleza kuwa wanawake wengi hawawaungi mkono waume zao kifedha, jambo ambalo limepelekea baadhi ya wanaume kujiingiza kwenye madeni yanayowafilishisha kiuchumi.
Hitmaker huyo wa “Akalulu” anaamini wanawake wanapaswa kutoa msaada zaidi katika mahusiano badala ya kujaribu kuwafurahisha wanaume kitandani kwani ngono ni jambo la ziada.
“Wanawake wengi siku hizi wanapenda ngono, hafla za birthdays na baby showers. Mambo haya yamepelekea wanaume wengi kufilisika kiuchumi. Wanawake wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuwasaidia waume zao. Siwezi mvumilia mwanamke ambaye anatoa ngono tu katika mahusiano,” Ziza Bafana alielezea.
Utakumbuka Ziza Bafana kwa sasa hana mpenzi anayejulikana kwa kuwa bado anamtafuta mwanamke wa ndoto yake.