
Mwimbaji nyota wa kike kutoka WCB, Zuchu anazidi kufanya vizuri kupitia digital platforms pamoja na kuongeza rekodi katika upande wa wasanii wa kike Afrika.
Kwa sasa Zuchu ni miongoni mwa wanamuziki wakike wenye idadi kubwa ya STREAMS katika mtandao wa Boomplay, hii ni baada ya kufikisha jumla ya streams Millioni 130 katika mtandao huo, hivyo anakuwa msanii wa pili Afrika baada ya Simi (Nigeria) mwenye streams 131.7
utakumbuka, Ijumaa ya wiki hii (Nov 18) Zuchu anatarajia kuanza tour yake ya muziki huko Marekani ambapo anatarajia kutumbuiza katika sherehe za utoaji wa tuzo za Afrimma 2022, pamoja na miji zaidi ya mitano.