
Staa wa muziki kutoka WCB, Zuchu, hatimaye amethibitisha kupokea malipo yake ya onyesho alilolifanya katika fainali za Mashindano ya CHAN yaliyofanyika nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa Instastory, Zuchu aliandika kuwa anashukuru mashabiki na watu wote waliowezesha ujumbe wake kufika kwa mashirika husika. Alisema kuwa tayari amepokea malipo yake yote na sasa anaendelea mbele na kazi zake.
Hii inakuja siku chache baada ya msanii huyo kuibua malalamiko mitandaoni akidai kuwa tangu atumbuize kwenye fainali hizo hakulipwa stahiki zake. Kauli yake ya sasa imeondoa sintofahamu na kuthibitisha kuwa suala hilo limepatiwa suluhisho.
Mashabiki wake wamefurahia kuona tatizo hilo limekwisha huku wengine wakimpongeza kwa uthubutu wa kulizungumza waziwazi.