Entertainment

Zuchu ashindwa kujizuia jukwaani baada ya show yake Houston Marekani kukosa watu

Zuchu ashindwa kujizuia jukwaani baada ya show yake Houston Marekani kukosa watu

Staa wa muziki wa Bongofleva Zuchu amewashukuru mashabiki zake wote waliojitokeza kwenye show yake huko Houston, Texas nchini Marekani licha ya idadi ndogo ya mashabiki kuhudhuria show hiyo.

Kupitia insta-story kwenye mtandao wa Instagram amesema kwamba kilichotokea kimempa hasira ya kufanya zaidi na anakubali kushindwa kama sehemu ya mafanikio yake.

“Nimejiuliza sana kwanini nilichagua kazi hii ya muziki lakini kwa matukio kama haya yananipa majibu kwamba wachache hutolewa kama mfano ili ije kuwa rahisi kwa wengine” aliandika Zuchu

Zuchu kwa sasa yupo kwenye ziara yake kimuziki (tour) nchini Marekani ambayo ilianza Novemba 18 hadi Desemba 3 mwaka huu.

Ziara hiyo ya Zuchu ni pamoja na kutumbuiza kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) zitakazotolewa Novemba 19 huko Dallas, Texas nchini Marekani ambapo Zuchu anawania kipengele cha Msanii Bora Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *