
Staa wa Bongo Fleva, Zuchu, amempa nyota tano dansa wake maarufu Ashurey akimtaja kuwa ndiye Dansa bora namba moja Afrika Mashariki kwa sasa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alipakia video ya Ashurey akifanya challenge ya wimbo wake mpya “Inama”, kisha akaandika ujumbe wa kumpa heshima kubwa kwa umahiri wake wa kucheza.
Wakati mashabiki wake wakiendelea kufurahia wimbo wake maarufu “Amanda”, Zuchu ametangaza kuwa yupo mbioni kuachia rasmi wimbo mpya uitwao “Inama”, akidai kuwa utafunika hata mafanikio ya hitsong yake, “Sukari”, ambayo imepata streams na views nyingi kwenye majukwaa ya kidigitali.
Tangazo hili limeongeza hamasa kwa mashabiki wake kote Afrika Mashariki, ambao sasa wanasubiri kwa shauku kuona iwapo “Inama” itavunja rekodi na kufikia viwango vikubwa zaidi ya nyimbo zake zilizopita.