
Mwanamuziki nyota kutoka lebo ya WCB, Zuchu, ameweka wazi hatua yake mpya nje ya muziki baada ya kudokeza ujio wa brand yake ya mavazi aliyoipa jina la Goo People Clothing Line.
Kupitia mitandao ya kijamii, Zuchu amefungua ukurasa rasmi wa Instagram wa brand hiyo ambapo amechapisha picha zake za kwanza akiwa amevalia T-shirt zenye maandishi “Amanda”. Hatua hii imeashiria kuwa msanii huyo anapanua upeo wake wa ubunifu na kuingia kwenye tasnia ya mitindo.
Mashabiki wake wamepokea habari hizi kwa shangwe, wengi wakimpongeza kwa kuonyesha mfano wa kuwekeza katika biashara sambamba na kazi yake ya muziki. Brand mpya ya Zuchu inatarajiwa kuvutia vijana na mashabiki wa muziki wake, huku ikimuweka kwenye ramani ya wasanii wa Afrika Mashariki wanaojitanua zaidi ya muziki.
Kwa sasa, bado haijafahamika lini mavazi kutoka Goo People Clothing Line yataanza kuuzwa rasmi, lakini mashabiki wanasubiri kwa hamu kutinga nguo hizo mpya zenye jina la msanii wao