Tech news

YouTube Kuanzisha Teknolojia ya Veo 3 Kuboresha Shorts

YouTube Kuanzisha Teknolojia ya Veo 3 Kuboresha Shorts

Kampuni ya YouTube imetangaza kuwa itaanza kutumia teknolojia ya akili bandia ya kisasa ya Veo 3, iliyotengenezwa na Google, ili kuboresha uzoefu wa watumiaji ndani ya kipengele chake cha video fupi, YouTube Shorts.

Teknolojia ya Veo 3 ni moja ya mifumo ya hali ya juu ya video AI ambayo inaweza kutengeneza, kuhariri na kusanifu video kwa kutumia amri rahisi za maandishi (text prompts), na inatambulika kwa uwezo wake wa kutambua rangi, sauti, muktadha, na mtiririko wa hadithi kwa usahihi wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Google, matumizi ya Veo 3 ndani ya YouTube Shorts yanalenga kusaidia watumiaji hasa wabunifu wa maudhui kuunda video zenye ubora wa juu kwa muda mfupi, bila hitaji la vifaa vya gharama kubwa au ujuzi wa kitaalamu wa uhariri.

Kupitia ushirikiano huo wa kiteknolojia, watumiaji wa YouTube Shorts wataweza kutumia AI kutengeneza transitions za kitaalamu, kuongeza athari za kuona (visual effects) kwa urahisi, kubadilisha maandishi kuwa video ya kipekee na kuboresha sauti, taa na rangi kiotomatiki.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za YouTube kuendelea kushindana na majukwaa kama TikTok na Instagram Reels, na pia kumrahisishia kila mtumiaji kuunda maudhui ya kuvutia kwa kutumia teknolojia ya kisasa.