Tech news

WhatsApp Yaboresha Njia ya Kuonyesha Replies

WhatsApp Yaboresha Njia ya Kuonyesha Replies

Kampuni ya Meta kupitia jukwaa la WhatsApp inafanya majaribio ya kuongeza mtindo mpya wa kuonyesha majibu yote yaliyotolewa kwenye meseji ambayo mtu amejibu. Hii ina maana kwamba badala ya kuona jibu moja tu, sasa mtumiaji ataweza kuona muktadha mzima wa mazungumzo yaliyotangulia yanayohusiana na meseji hiyo.

Kipengele hiki kinatarajiwa kusaidia watumiaji kuelewa kwa urahisi zaidi muktadha wa majibu hasa katika mazungumzo ya vikundi ambapo mazungumzo yanaweza kuwa mengi na kuchanganyika. Hii itapunguza kuchanganyikiwa na kuifanya mazungumzo yawe wazi na rahisi kufuatilia.

Hadi sasa, WhatsApp bado inajaribu mtindo huu na imetolewa kwa baadhi ya watumiaji wa toleo la majaribio (beta). Haijatangazwa rasmi lini kipengele hiki kitawekwa kwa watumiaji wote.

Mtumiaji anayetaka kujaribu awali anaweza kujiunga na programu ya WhatsApp Beta kupitia duka la programu la simu yake.