Entertainment

SPICE DIANA AFUNGUKA SIRI YA MUZIKI WAKE KUPENYA TANZANIA

SPICE DIANA AFUNGUKA SIRI YA MUZIKI WAKE KUPENYA TANZANIA

Mwanamuziki Spice Diana ni miongoni mwa wasanii wachache kutoka Uganda waliofanikiwa kupenya kwenye soko la muziki nchini Tanzania.

Akizungumza kuhusu kufanya kazi na wasanii wa Tanzania, mrembo huyo amesema huwa hatumii pesa nyingi kwenye kolabo kwani kigezo kikubwa ambacho yeye hutumia ni kuwakodisha waongozaji wazuri wa muziki wanaopendwa na wasanii wa Tanzania.

Hitmaker huyo wa “Body” amesema kufanya kazi nao kumesaidia kutangaza nyimbo zake nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kwa sasa Spice Diana anafanya poa na singo yake mpya iitwayo “Upendo” ambayo amemshirikisha msanii wa Bongofleva, Zuchu.

Kando na Zuchu,  Spice Diana amefanya kazi na Rosa Ree pamoja na Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *