Rapa kutoka nchini Marekani Drake ameingia kwenye headlines baada ya kununua chanuo la gharama zaidi aina ya Rolls Royce Brush kwa ajili ya kuchania nywele zake .
Chanuo hilo ambalo limenakshiwa kwa Led Lights linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola million 1.1 ambazo ni zaidi ya shilling million 122 za Kenya.
Hii si mara ya kwanza kwa mtu mzima Drizzy kumiliki vitu vya gharama kubwa ,kwani amewahi kuripotiwa kumiliki kitanda chenye gharama ya zaidi ya million 44.5 kilicho nakshiwa na manyoya ya farasi na vipande vya baadhi ya madini.