Lebo ya Sol Generation imetangaza kumsaini msanii Bien Aime Baraza kwa mkataba wa shillingi millioni 50.
Mkataba wa msanii huyo utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu na umekuja wakati huu wasanii wa kundi la Sauti Sol wamezindua mpango wa kuachia kazi zao kama wasanii wa kujitegemea.
Sauti Sol kama kundi bado limesainiwa kwenye lebo ya Universal Music lakini Bien amejiunga na Sol Generation kama msanii wa kujitegemea.
Bien anaungana na msanii Bensoul pamoja na Nviiri The Storyteller ambao wamekuwa wakitamba katika tasnia ya muziki nchini na nyimbo kama, Nairobi na Niko Sawa.
Kusaini kwa Bien kwenye lebo ya sol generation inakuja mra baada ya msanii huyo kuachia EP yake mpya iitwayo Bald Men Love Better, iliyomshirikisha mpiga kinanda maarufu nchini Aaron Rimbui