Entertainment

PENZI LA MICHAEL B. JORDAN NA LORI HARVEY LAVUNJIKA

PENZI LA MICHAEL B. JORDAN NA LORI HARVEY LAVUNJIKA

Penzi la Muigizaji wa Filamu kutoka Marekani Michael B. Jordan na Lori Harvey limefikia mwisho.

Wawili hao wameachana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja na nusu.

Kwa mujibu wa Jarida la People, sababu ya kuachana kwao imeelezwa kuwa ni utofauti wa umri kati yao.

Kupishana miaka 10 kumemfanya Michael B. Jordan (35) kuwa na hamu ya kutaka kutulia na kupata mwenza wa milele huku Lori Harvey (25) akiwa bado anataka kukula bata.

Utakumbuka mwaka wa 2020 Mwanamitindo Lori Harvey ambaye ni mtoto wa mchekashaji maarufu nchini Marekani Steve Harve, aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na Rapa Future.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *