Entertainment

Femi One awajibu wanaowapinga wasanii kutumbuiza kwenye majukwaa ya kisiasa

Femi One awajibu wanaowapinga wasanii kutumbuiza kwenye majukwaa ya kisiasa

Rapa Femi One ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya “Lip Service” amechukizwa na kitendo cha wakenya kuwakosoa wasanii wanapotumbuiza kwenye mikutano ya kisiasa.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Membo huyo amesema wasanii wanapoalikwa kufanya shows kwenye majukwaa ya kisiasa haimaanishi wanaunga mkono sera za viongozi wa mirengo fulani bali wameenda pale kwa ajili ya kujitafutia riziki.

Utakumbuka Femi One ni moja kati ya wasanii waliotumbuiza kwenye majukwaa ya kisiasa hapa nchini Kenya msimu wa kampeini za uchaguzi mkuu uliokamilika, akiupigia upata mrengo wa Azimio la Umoja ambao ulishindwa na muungano wa Kenya Kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *