Sports news

CHAN 2024 Yapumzika kwa Siku Mbili, Robo Fainali Kuanza Ijumaa

CHAN 2024 Yapumzika kwa Siku Mbili, Robo Fainali Kuanza Ijumaa

Mashindano ya Soka ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN) 2024 yameingia katika mapumziko mafupi ya siku mbili, leo na kesho, baada ya kipindi cha siku 17 za mechi za hatua ya makundi zilizoshuhudia ushindani mkali kutoka kwa timu shiriki. Mapambano hayo yanatarajiwa kurejea Ijumaa hii kwa hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali, Harambee Stars ya Kenya itashuka dimbani kuchuana na Madagascar kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi. Kenya ilifuzu hatua hiyo kwa kishindo baada ya kuongoza Kundi A kwa alama 10. Madagascar kwa upande wao, walijikatia tiketi kwa kumaliza nafasi ya pili katika Kundi B kwa alama 7, nyuma ya Tanzania.

Mechi ya pili ya robo fainali Ijumaa hiyo hiyo, itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wenyeji Tanzania watawakaribisha Morocco. Tanzania walifuzu kwa kuongoza Kundi B kwa alama 10, wakizidi Madagascar kwa alama tatu. Morocco walimaliza nafasi ya pili katika Kundi A kwa alama 9, alama moja nyuma ya Kenya.

Robo fainali hizi zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku macho ya wengi yakiwa kwa timu za Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania, ambazo zimeonesha kiwango bora hadi sasa katika mashindano haya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *