Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Zuchu, amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikidai kwamba hatoshirikiana na wasanii wa Kenya kwa sababu ya madai ya Wakenya kumtusi Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Kiss 100, Zuchu ameeleza kuwa hajawahi kutoa kauli hiyo na kusisitiza kuwa habari hizo hazina ukweli wowote. Amesema kuwa taarifa hizo zilitungwa kwa lengo la kumharibia jina na kumkosanisha na mashabiki wake wa Kenya.
Zuchu ameweka wazi kuwa hana nia yoyote mbaya kwa wasanii wa Kenya, bali anawaheshimu kwa vipaji vyao. Ameeleza pia kuwa tayari ameshirikiana nao kwenye miradi yake ya muziki, wakiwemo wasanii wa kundi la Hart the Band, waliopata nafasi kwenye albamu yake.
Taarifa hizo ziliibuka muda mfupi baada ya Zuchu kuwasili Kenya kwa ajili ya kutumbuiza leo kwenye fainali za CHAN 2024 katika uwanja wa Kasarani, ambapo atashiriki jukwaa moja na wasanii wengine wakubwa akiwemo Savara na Eddy Kenzo.
Kauli yake sasa imeweka wazi msimamo wake na kumaliza tetesi zilizokuwa zikisababisha mjadala mkali mitandaoni kuhusu mahusiano ya muziki kati ya Tanzania na Kenya, akisisitiza mshikamano na ushirikiano wa kisanaa badala ya mgawanyiko.
Baadhi ya wadau wa michezo na mashabiki wamehoji iwapo pesa hizo zitatolewa, huku wengine wakisisitiza kuwa wasanii wanapaswa kuwa makini na ahadi wanazotoa kwa umma ili kuepusha migongano na kuharibu taswira ya michezo nchini.