Baby Mama wa Mchekeshaji Mulamwah, Ruth K, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kujibu kwa kejeli habari za aliyekuwa mpenzi wake, kuonyesha hadharani mpenzi wake mpya anayefahamika kama Emillianah.
Kupitia mitandao ya kijamii, Ruth amemwonya Emillianah dhidi ya kuzaa mtoto na Mulamwah, akisisitiza kuwa mchekeshaji huyo ana historia tata linapokuja suala la malezi ya watoto. Ameonyesha wazi kwamba ingawa hawezi kupinga uhusiano wao, suala la kupata mtoto linaweza kuwa changamoto kubwa kwa upande wa Emillianah.
Kauli hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki. Wengi wamechukulia ujumbe huo kama dongo kwa Mulamwah ambaye tayari ana mtoto na Ruth, huku changamoto za malezi zikiwa zimewahi kujadiliwa sana mtandaoni.
Mashabiki wengine waliunga mkono msimamo wa Ruth wakimtaka Emillianah kuwa makini, huku wengine wakimshutumu Ruth kwa kuingilia maisha mapya ya Mulamwah kwa kuonyesha wivu wa kimapenzi.