Youtuber maarufu nchini Kenya, Mungai Eve, ametoa onyo kali kwa mwanaume asiyejulikana anayedaiwa kuendelea kumtaja na kuingiza jina lake kwenye mabishano ya hadharani mtandaoni.
Mungai Eve, kupitia mitandao yake ya kijamii, amesema wazi kuwa hatasita kuwasilisha ushahidi dhidi ya mtu yeyote atakayejaribu kumfanya aonekane duni au kumtuhumu bila sababu. Amesisitiza kuwa utulivu wake wa sasa haupaswi kuchukuliwa kama udhaifu, bali ni ishara ya uthabiti na busara ya kukabiliana na changamoto.
Kauli hiyo imetajwa na mashabiki kuwa jibu kwa ex wake, Trevor, ambaye juzi kati alimtaka aombe radhi kwa Wakenya kutokana na matamshi yake kwamba hawezi kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye kipato chake kiko chini ya shilingi laki tano za Kenya.
Trevor alitoa kauli hiyo baada ya wafuasi kumshauri amsaidie Eve, ambaye amekuwa akikabili changamoto mbalimbali za kimaisha tangu kuvunjika kwa uhusiano wao.