Tech news

Apple Yarekebisha Button ya Kuzima Alarm Baada ya Malalamiko ya Watumiaji

Apple Yarekebisha Button ya Kuzima Alarm Baada ya Malalamiko ya Watumiaji

Kampuni ya Apple imetangaza mabadiliko mapya katika mfumo wake wa uendeshaji wa simu, iOS, kufuatia malalamiko kutoka kwa watumiaji waliokuwa wakikerwa na urahisi wa kuzima alarm kwa bahati mbaya.

Katika toleo la awali la iOS 26, Apple ilikuwa imefanya button ya kuzima alarm kuwa kubwa zaidi na rahisi kutumia kwa single tap, jambo ambalo lilisababisha baadhi ya watu kuizima alarm wakiwa bado usingizini bila hata kujua.

Watumiaji wengi waliibua malalamiko mtandaoni, wakisema kwamba walikuwa wanazima alarm bila kukusudia, hali iliyowachelewesha shughuli zao au hata kukosa kuamka kwa wakati.

Kufuatia hali hiyo, Apple sasa imefanya mabadiliko katika toleo linalofuata iOS 26.1. Katika toleo hilo, button ya kuzima alarm haitabofya kwa “tap” ya kawaida tena, bali itahitaji ku-slide ili kuzima alarm. Hii ni hatua iliyolenga kuhakikisha kwamba mtumiaji anafanya uamuzi wa makusudi kuzima alarm, na siyo kwa kugusa simu kwa bahati mbaya akiwa usingizini.

Aidha, Apple imesema kuwa slide hiyo imeundwa kuwa na sensitivity maalum, ili kupunguza uwezekano wa mtu kuiamsha au kuizima alarm kwa urahisi bila kutarajia.

Mabadiliko haya ni sehemu ya juhudi za Apple kuboresha uzoefu wa mtumiaji kwa kuzingatia maoni kutoka kwa jamii ya watumiaji wake duniani kote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *