Kampuni ya Meta imetangaza kuwa Instagram ipo mbioni kuanzisha mpangilio mpya wa tabs kwenye app hiyo maarufu, katika juhudi za kuboresha matumizi na kuongeza ufanisi kwa watumiaji.
Katika mabadiliko hayo mapya, watumiaji wataweza ku-swipe kwenda kushoto au kulia kubadilisha tabs, ikiwa ni pamoja na sehemu za Home, Reels, DMs (Direct Messages), na Search. Mpangilio huu mpya unalenga kupunguza idadi ya mibofyo (clicks) na kufanya urambazaji ndani ya app kuwa wa haraka na wenye mtiririko rahisi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Instagram, style hii mpya inafanana kwa kiasi fulani na muundo wa TikTok, ambao umejizolea umaarufu kutokana na interface yake nyepesi na ya kisasa. Watumiaji wataweza kufikia sehemu wanazozitumia mara kwa mara kwa urahisi zaidi kama vile kutazama video fupi (Reels), kutuma ujumbe, au kufanya utafutaji ndani ya app.
Mabadiliko haya yanakuja wakati Instagram ikiendelea kujiboresha kukabiliana na ushindani mkali kutoka kwa majukwaa mengine ya kijamii kama TikTok na Snapchat, huku ikilenga kuwapa watumiaji wake uzoefu wa kisasa, unaozingatia urahisi na kasi.
Instagram haijatangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa mabadiliko haya kwa watumiaji wote, lakini maboresho haya yanatarajiwa kuanza kutekelezwa hatua kwa hatua katika masasisho yajayo ya app.