Mkali wa Rap kutoka Kenya, Khaligraph Jones, amewatolea uvivu wakosoaji wanaobeza mtindo wake wa mavazi, akisema yeye si mtu wa kuvaa kiholela kama wanavyodhani.
Kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, rapa huyo ameonyesha wardrobe yake yenye mavazi ya aina mbalimbali, akibainisha kuwa kila vazi analolichagua linaendana na tukio au wakati husika.
Khaligraph amesema kuwa watu wengi wanaomkosoa hawajui gharama ya mavazi anayovaa, kwani mengi ni ya thamani kubwa na yanawakilisha hadhi yake kama msanii wa kimataifa.
Papa Jones ameongeza kuwa mtindo wake wa mavazi ni sehemu ya utambulisho wake katika muziki na kwamba anapenda kuonyesha ubunifu na umaridadi bila kuiga mtu yeyote.