Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Harmonize, ameungana na viongozi na mashabiki mbalimbali kutoka Afrika Mashariki kutuma salamu za rambirambi kwa Wakenya kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.
Kupitia Insta Stories zake, Harmonize amerepost ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan akieleza masikitiko yake juu ya kifo hicho, na akaambatanisha na ujumbe wake wa kuonesha mshikamano na wananchi wa Kenya.
Katika ujumbe huo, Harmonize ameonesha huzuni na upendo kwa Wakenya akiwafariji kwa kumpoteza kiongozi huyo, akisema yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya siku saba yaliyotangazwa na Rais William Ruto.
Msanii huyo amesema tukio hilo limegusa hisia za wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki, akisisitiza umuhimu wa umoja na udugu miongoni mwa mataifa jirani katika nyakati za huzuni.