Entertainment

Eric Omondi Akanusha Vikali Tuhuma za Kutoa Kafara Shalkidoh

Eric Omondi Akanusha Vikali Tuhuma za Kutoa Kafara Shalkidoh

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi amefunguka kwa uchungu baada ya tuhuma zilizozagaa mtandaoni zikidai kuwa alimtoa kafara msanii Shalkidoh aliyezikwa jana nyumbani kwao kaunti ya Kiambu.

Akizungumza kufuatia tetesi hizo, Eric amekanusha vikali madai hayo, akisema ni uvumi wa kupotosha unaolenga kuharibu jina lake na juhudi zake za kusaidia watu. Amesema kuwa hajawahi kujihusisha na mambo ya ushirikina bali anatenda mema kwa nia ya dhati kusaidia jamii.

Eric ameongeza kuwa maneno ya watu hayawezi kumkatisha tamaa, na ataendelea kuwasaidia Wakenya wenye uhitaji bila kuogopa maneno ya chuki au fitna.

Hata hivyo amesema lengo lake ni kuona vijana wanapata fursa bora za maisha kupitia miradi na kampeni zake za kijamii, akisisitiza kuwa atabaki kuwa sauti ya matumaini kwa waliokata tamaa.

Kauli ya Eric Omondi imekuja mara baada ya walimwengu mtandaoni kudai kuwa huenda mchekeshaji huyo alihusika na kifo cha Shalkidoh, ikizingatiwa kuwa pikipiki aliyompa kama msaada ndiyo iliyosababisha ajali iliyomtoa uhai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *