Entertainment

Rapa Khaligraph Alia Kwa Uchungu Kufuatia Kifo cha Raila

Rapa Khaligraph Alia Kwa Uchungu Kufuatia Kifo cha Raila

Rapa wa Kenya, Khaligraph Jones, ameeleza majonzi makubwa kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga, akisema amebaki bila maneno ya kuelezea machungu anayoyapitia.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Khaligraph amekiri kuguswa sana na taarifa za kifo cha Raila, akieleza kuwa tangu jana amekuwa akihangaika kuamini kilichotokea.

Rapa huyo wa ngoma ya “Ting Badi Malo”, amesema kifo hicho kimemwacha akiwa amevunjika moyo kabisa, akiongeza kuwa Raila atabaki kuwa shujaa wake wa milele..

Khaligraph, ambaye amewahi kumtaja Raila kama kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika maisha yake na kwa vijana wengi, amesema urithi wa Baba Raila utaendelea kuishi kupitia vizazi vinavyokuja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *