Kampuni ya Snapchat imezindua rasmi kipengele kipya kinachoitwa “AI Mode”, ambacho kinalenga kubadilisha kabisa jinsi watumiaji wake wanavyopiga na kurekodi picha na video. Kwa mara ya kwanza, watumiaji wa Snapchat sasa wataweza kuchukua Snaps zenye ubora wa hali ya juu (HD Quality) kwa kutumia nguvu ya inteligensia bandia (AI).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, AI Mode ni teknolojia ya kisasa inayotumia algorithms za akili bandia kuboresha mwangaza, utofautishaji wa rangi (contrast), na utulivu wa picha (stabilization) kwa wakati halisi hata katika mazingira ya mwanga mdogo au harakati nyingi.
Watumiaji wataweza kuwasha kipengele hiki kupitia kamera ya Snapchat kwa kubonyeza kitufe cha “AI” kilicho juu ya skrini, ambapo mfumo utaanza kuchakata picha kwa kutumia akili bandia.
Snapchat imethibitisha kuwa AI Mode inazinduliwa kwa awamu, ikianza na watumiaji wa iOS (iPhone 13 na kuendelea), huku Android ikifuata mwezi ujao. Hii inatarajiwa kuongeza ushindani dhidi ya mitandao kama Instagram na TikTok ambao tayari wanafanyia kazi teknolojia za video na picha za hali ya juu.