Sports news

Ligi Kuu England: Manchester United Yaizamisha Liverpool Anfield Kwa Mabao 2-1

Ligi Kuu England: Manchester United Yaizamisha Liverpool Anfield Kwa Mabao 2-1

Manchester United wamepata ushindi muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Liverpool mabao 2-1 katika dimba la Anfield, Jumapili usiku.

United walianza kwa kasi, wakipata bao la mapema dakika ya 2 kupitia Bryan Mbeumo, ambaye alitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Liverpool na kumtungua kipa Alisson Becker kwa shuti kali.

Liverpool walijibu mashambulizi mara kwa mara kipindi cha pili na hatimaye kusawazisha dakika ya 78 kupitia Cody Gakpo baada ya ushirikiano mzuri na Federico Chiesa.

Hata hivyo, matumaini ya wenyeji yalikatishwa dakika ya 84 baada ya Harry Maguire kuifungia Manchester United bao la ushindi kwa kichwa kizuri kufuatia kona ya Bruno Fernandes.

Kwa matokeo hayo, Manchester United wanapanda hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 13, huku Liverpool wakishikilia nafasi ya nne na pointi 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *