Msanii wa muziki kutoka Kenya, Willy Paul, amewashangaza mashabiki wake baada ya kufichua kwamba hana mpango wa kuoa, licha ya kuwa na moja ya nyimbo kubwa zaidi katika taaluma yake inayotumika sana kwenye harusi.
Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Willy Paul amesema kuwa kiwango cha usaliti katika mahusiano ya siku hizi kimemfanya apoteze imani katika ndoa.
Kwa mujibu wake, watu wengi wamekuwa wakisaliti wenza wao, jambo ambalo limeharibu maana halisi ya upendo wa kweli.
Msanii huyo ambaye amewahi kutoa nyimbo kadhaa za mapenzi, ikiwemo wimbo wa “Yes I Do” unaotumika sana kama wedding anthem, amesema kuwa licha ya mafanikio yake katika muziki wa mapenzi, hana mpango wa kuingia kwenye ndoa kwa sasa.
Willy Paul amesema anachagua kuzingatia kazi yake ya muziki badala ya kuhusisha maisha yake binafsi na ndoa ambayo, kwa mtazamo wake, si imara tena katika kizazi cha leo.