Mtangazaji na mchekeshaji Oga Obinna ameonyesha heshima zake za mwisho kwa hayati Raila Odinga kwa kunyoa kipara kamili, kama ishara ya maombolezo na heshima kulingana na tamaduni za jamii ya Wajaluo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obinna ameposti picha akionyesha kichwa chake kilichonyolewa kabisa, akifafanua kuwa kitendo hicho kilikuwa njia yake ya kumuenzi kiongozi huyo aliyegusa maisha ya wengi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa mila za Kijaluo, kunyoa kipara ni ishara ya huzuni, heshima, na mshikamano na familia ya aliyeaga dunia wakati wa msiba.
Kitendo hicho kimezua maoni mengi mtandaoni, wengi wakimsifu Obinna kwa kuenzi utamaduni wa Kiafrika na kuonyesha mshikamano na Wakenya wanaoendelea kuomboleza.