Tech news

Firefox Yazindua Mfumo Mpya wa Kuficha IP Kama Safari ya Apple

Firefox Yazindua Mfumo Mpya wa Kuficha IP Kama Safari ya Apple

Kampuni ya Mozilla, watengenezaji wa kivinjari cha Firefox, imepiga hatua kubwa katika kulinda faragha ya watumiaji wake kwa kuzindua mfumo mpya unaoitwa Firefox VPN, unaolenga kuficha anuani ya IP (IP address) na kulinda taarifa binafsi za watumiaji wanapoperuzi mtandaoni.

Mfumo huu mpya unaiga dhana inayofanana na Private Relay ya Apple, ambayo ipo kwenye kivinjari cha Safari. Kupitia Firefox VPN, taarifa zote za utumiaji wa mtandao zitapitia kwenye seva maalum za VPN za Mozilla, jambo litakalofanya iwe vigumu kwa tovuti au huduma nyingine mtandaoni kujua IP ya mtumiaji, eneo lake halisi au shughuli anazofanya.

Aidha, mfumo huo utaweka kizuizi kwa waendeshaji wa huduma za intaneti (ISP) kama vile mitandao ya simu na watoa huduma za intaneti, kuzuia uwezo wao wa kuona tovuti ambazo mtumiaji amefungua au shughuli zake anazofanya mtandaoni.

Mozilla imeeleza kuwa huduma hii itatolewa bure kabisa, na itakuwa na mwendo wa kasi sawa na wa kawaida wa intaneti, au hata zaidi. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa lengo la huduma hiyo si kutoa huduma kamili ya VPN ya kubadili eneo (location), bali ni kulinda faragha na usalama wa taarifa za mtumiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *