Sports news

Bingwa wa Dunia wa Fedha, Daniel Ebenyo, Kutafuta Taji la Kitaifa Eldoret

Bingwa wa Dunia wa Fedha, Daniel Ebenyo, Kutafuta Taji la Kitaifa Eldoret

Mwanariadha aliyeshinda medali ya fedha ya dunia katika mbio za mita 10,000 mwaka mwaka 2023 Daniel Simiu Ebenyo ananuia kutwaa taji ya kitaifa atakaposhiriki katika mashindano ya kitaifa ya mbio za nyikani yatakayoandaliwa katika uwanja wa kilabu cha michezo cha Eldoret Jumamosi hii. Ebenyo, alishinda mbio za mwaka jana mbele ya Nickson Kogei na Simon Mungai.

Wanariadha wengine watakaoshiriki ni pamoja na Ishmael Kipkurui Rokitto, Benson Kiplangat wa South Rift, na Emmanuel Kipchumba wa KDF miongoni mwa wengine. Kinyang’anyiro cha wanawake kitajumuisha Maurine Jepkoech Chebor wa Kenya Police, ambaye ananuia kuandikisha ushindi baada ya kumaliza ya pili mwaka jana nyuma ya Brillian Jepkorir Kipkoech, aliyetwaa taji ya wanawake.

Mbali na ushindani wa majina makubwa, mashindano haya pia yatatumika kuchagua wanariadha watakaoiwakilisha Kenya katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyikani, yatakayofanyika tarehe 10 Januari 2026 mjini Tallahassee, Florida, Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *